Total Onslaught - Swahili
231SW - Kilio Kikuu
Added: 30th September 2014
Views: 2938
Comments: 0
Kilio kikuu ni fundisho la ufunuo 18. Inazungumzia matukio ya siku za mwisho kabisa ambayo mungu anaeleza jinsi uharibifu wa nguvu hizi zilizo tawala matukio za kisasa ulimwenguni. Tunatazama ulimwengu wa muziki, uchumi, dini, burudani, na tunagundia zote zinakubaliana. Katika hotuba hii, agenda zao ficho zinawekwa wazi. Kilio kikuu ni kilele cha onyo hili kwa ulimwengu na inafuatiliwa na kuingiliwa kati kwa mungu kwa mambo ya wanadamu.

232SW - Mwaka wa 1844 na Mashambulizi Jumla
Added: 30th September 2014
Views: 3485
Comments: 0
Filamu hii inazungumzia kumalizika kwa unabii wa siku 2300 wa danieli 8 na 9. Inaonyesha kwamba uhasama ule ule uliyomalizikia kwa kumsulubisha kristo utaonekana tena katika kufunga historia ya dunia. Katika mapito ya vikundi vya siri na mafikara ya wana new age, kuna mwamko wa kuwaharibu wale wanaoamini katika wokovu wa kristo yesu pekee na uhalali wa neno lake. Ushahidi unaonyeshwa wa mipango yao kuondolea mbali wale ambao wanaisimamia kweli na haki.

233SW - Ishara na Maajabu
Added: 6th October 2014
Views: 3108
Comments: 0
Biblia inatuonya kuhusu ishara na maajabu yatakayofanywa katika siku za mwisho kuwadanganya hata ikiwezekana wale wateule. Matukio makuu ya wakati wetu jinsi yalivyofanyika kupitia wana new age yanaonyeshwa katika filamu hii. Mafundisho ya mwonekano yanalinganishwa na yale ya biblia. Mitazamo miwili ya mpambano kati ya nguvu pinzani za siku za mwisho kama yalivyo katika kitabu cha ufunuo yanalinganishwa. Je haya yanatupeleka wapi Na mada kuu ni ipi?

234SW - Historia Kufikia Kilele
Added: 30th September 2014
Views: 3226
Comments: 0
Kurudi kwa kristo mara ya pili kumetabiriwa katika biblia na kwa karne nyingi watu wamesubiri tukio hili kubwa. Je biblia inasema nini kuhusu fundisho hili kinyume na mafundisho mengi katika ulimwengu wa leo. Je kuna unyakuzi wa siri? Je ni nini kitawatokea wafu kristo anaporudi? Maswali haya na mengine mengi yanajibiwa katika fundisho hili. Kuingilia kati huku kwa mungu kwa maswala ya binadamu inahalalisha wale waliosimamia kweli na haki yake.

235SW - Millennia Iliyo Subiriwa Sana
Added: 30th September 2014
Views: 3076
Comments: 0
Dunia inasubiri millennia ya amani ambapo kristo atausimamisha ufalme wake na uovu wote utakoma. Je tutakaribisha millennia lini? Je biblia inafundisha nini kuhusu millennia ambapo watakatifu watahukumu ulimwengu? Je hii inalinganishwaje na fundisho kwamba dunia nzima itaongoka na kubadilika? Haya ndiyo mambo yanayobainishwa hapa. Tunapewa mtazamo mdogo wa dunia mpya na ufalme wa kristo. Hakutakuwepo na kifo wala uchungu wala mateso.

236SW - Mwaliko Mkuu
Added: 30th September 2014
Views: 2766
Comments: 0
Mwaliko mkuu ni kusalimu yote na kumfuata kristo. Yesu aliamuru wanafunzi wake kuhubiri injili na kuwabatiza walioamini kwa jina la baba, mwana, na roho mtakatifu. Je alikuwa akizungumzia ubatizo wa watoto au watu wazima? Je kuna kubatizwa kwa moja kwa moja, kunyunyiziwa maji, kumwagiwa maji, kuzamishwa au haijalishi? Je bibilia inalofundisho gani kuhusu swala hili tata- kusherehekea kufufuka kwa kristo.

-