|
|
Katika DVD hii kuinuka kwa mfumo mpya duniani inajadiliwa, na athari zake kisiasa kiuchumi na katika jamii. Njama hii inayotaka kushurutisha namna ya kuwaza kwa binadamu inawekwa wazi. Matukio yanayopelekea kuwepo kwa mambo haya kama vile ugaidi, vita dhidi ya kile wanachokiita “muungano mwovu” inajadiliwa na jinsi mambo haya yata adhiri maisha yako binafsi.
|
|
Je wafu huenda wapi? Je bibilia inafundisha nini kuhusu jambo hili? Je kuzimu ipo? Mbingu ya saba? Maisha baada ya kufa? Kuzaliwa tena baada ya kufa? Roho za waliokufa? Je biblia inazungumzia umizimu? Gundua ukweli kuhusu mafundisho ya kweli ya biblia kwa mada hii tata.
|
|
DVD hii inaeleza njia ambazo vikundi tofauti vinavyojiita vyama vya kikristo wanaendesha matukio ya kiroho ilikutayarisha njia ya kuja kwa kristo wa kimataifa anayekidhi haja za dini zote. Vuguvugu la Christian science, umormon, wajehovah witnesses, na wana new age wanawekwa wazi. Hapa pia matreya anachunguzwa na mafundisho yake yaliyo kinyume na biblia na kuonekana kwa kristo wa uongo katika dunia ya sasa. Je new age inaathiri maisha ya kimizimu tuu au pia maisha ya kawaida katika mifumo ya ...
|
|
Katika zama ya kuvumiliana kidini na muungano , uhasama wa zamani unazikwa. Makanisa yanaungana yaliyokuwa yametenganishwa na maswala ya mafundisho. Je maendeleo haya yana msingi wowote kimaandiko au ni kanuni za kibinadamu. Je kweli inatolewa kafara kwa sababu ya umoja? Je tunaingia katika kipindi cha amani ambayo biblia inatuonya? DVD hii inatazama pia falsafa ya wahubiri wakuu kama vile Robert schuller na wengine.
|
|
Moto wa ajabu inazungumzia miujiza yanayopatikana katika ibada za sasa za kikristo.mwanzo na mbinu za makanisa haya makubwa na mwanzo wao wa haja inajadiliwa na kuwekwa wazi. Je chanzo cha msukumo wao ni upi? Je ni kwa mtungi upi wanapochota maji yao? Je wahubiri wakubwa kama vile schuller, hybels, Rick warren, Copeland, Hinn etc. wanakwenda wapi na falsafa zao? Katika Video hii utagundua kuwa theologia ya kisasa imebadilika kutoka kwa mtazamo wa mungu hadi kwa mtazamo wa kibinadamu, kutoka k...
|
|
Je umoja wa mataifa ina agenda ya kisiasa tuu ? au ina mtazamo wa kidini katika kazi zake? Katika Video hii agenda zake ficho yanawekwa wazi. Kuanzia wakati ilipoanzishwa, lengo lake kuu limekuwa kuunda mfumo mmoja wa kisiasa na wakidini iliyo na athari kwa kila mtu katika ulimwengu na matokeo ya kudhuri kwa wale ambao tumaini lao ni kwa wokovu wa Kristo pekee yake.
|
|
Pambano kuu kati ya Kristo na Shetani katika vizazi vyote jinsi ilivyo elezwa katika ufunuo 12 inatolewa. Chuki aliyonayo Lusifa dhidi ya mwana wa mungu na hao watoto wanao kubali kuongozwa naye imepelekea kuwa na umwagikaji mkubwa wa damu, uchungu na mateso katika sayari hii isiyoweza kufirika. Mateso ya wale wote waliyo iamini Biblia katika zama zaziga na migogoro ya mwisho itakayokuja juu ya dunia yanaonyeshwa katika video hii.
|
|
Ni fundisho la ufunuo sura ya 10 inayo onyesha kinyume ya mnyama ambaye anazuka kutoka katika shimo la kuzimu (ufalme wa giza). Inaweka wazi shirika ambalo mungu analiinua ili kusimama didhi ya makosa mengi ambayo shetani ameyaweka ulimwenguni kumnyang’anya mwanadamu wokovu. Shiriki limetiwa nguvu na ujumbe maalum ya kuonya nalo linazuka wakati mwafaka katika unabii wa biblia kutangaza injili ya milele ya wokovu katika kristo na kuwa waminifu katika neno lake.
|
|
Moja ya sifa ya kutofautisha shirika litakalo kabiliana na ufalme wa shetani jinsi ambavyo imeelezwa katika ufunuo 12 na 14 ni kwamba wana ushuhuda wa yesu iliyoelezwa kama roho ya unabii. Je mungu anazungumza na mwanadamu wa sasa? Kati ya manabii wengi wanaodai kuwa wanao ujumbe kutoka kwa mungu , je tunayo sauti kutoka katika kiti cha rehema? Je wawezaje kutambua nabii wa kweli? Je biblia inatuonyesha nini kuhusu mada hii?
|
|
Ni fundisho la ufunuo 14, ikiwa ni onyo la mwisho kwa ulimwengu. Ujumbe wa malaika watatu ilivyoelezwa wazi kama inayokabiliana na ufalme inayowekwa na wakuu wa kidini na kisiasa wa wakati wetu. Hili ni onyo kuu kuwahi kuwepo na inaishia katika kurudi mara ya pili kwa kristo. Kila mmoja anapashwa kujua kilichoko katika ujumbe huu.
|
|