Total Onslaught - Swahili
211SW - Siri Kuhusu Vikundi Vya Siri
Added: 29th September 2014
Views: 3618
Comments: 0
Mengi yameandikwa kuhusu vikundi vya siri na uvumi mwingi kuhusu nguvu inayoyadhibiti. Asili ya usiri ni kwamba mamlaka hasa nyuma ya nguvu hizi lazima ibakie siri. Katika hotuba hii, ushahidi bayana inatolewa kuonyesha ninani anayesimama nyuma ya kiti cha enzi cha uwezo duniani.

212SW - Mipango Ya Siri
Added: 29th September 2014
Views: 3075
Comments: 0
Inafichua falsafa ya vikundi vya siri. Inadhibitisha bayana kutoka katika vianzo bora kwamba mungu anayeabudiwa katika madhabahu ya siri sio Mungu wa biblia. Jifundishe kuhusu ushahidi huu mwenyewe na udhibitishe kama kweli mambo haya ni jinsi yalivyo.

213SW - Vita Vya Biblia
Added: 29th September 2014
Views: 3263
Comments: 0
Kupigana kwetu sio dhidi ya damu na nyama. Majeshi ya kiroho yangependa kumwibia mwanadamu chanzo pekee cha msukumo ikionyesha njia ya kufikia wokovu. Katika vita vya biblia ushahidi mzito unatolewa jinsi ambavyo adui anafanyakazi kwa usiri kutengeneza hatua za mashambulizi yake ya mwisho kwa neno la Mungu. Historia kuhusu waliopanga njama hii ya kulibadilisha neno la Mungu ili iambatane na falsafa yao ya kimashetani yanawekwa wazi.

214SW - Kulibadilisha Neno
Added: 29th September 2014
Views: 2584
Comments: 0
Katika filamu hii inaonyeshwa jinsi ambavyo biblia imebadilishwa kupitia matoleo mapya ikiwa na lengo la kumnyanganya kristo ukuu wake. Hebu tazama na ukaone kama ni kweli.

215SW - Mapinduzi, Madikteta na vitaMapinduzi Madikteta na Vita
Added: 29th September 2014
Views: 3057
Comments: 0
Mapinduzi madikteta na vita vinahitaji kufadhiliwa na kuungwa mkono ili zifanikiwe. Je ninani aliyenyuma ya moto huu ambayo umewahangaisha wanadamu hasa katika karne iliyopita.? Je nguvu hizi za giza zinafanya kazi kisiri ilikufikia lengo lao la makubaliano ya kifilosofia ya kimachafuko (Hegelian philosophy) ili kuleta mfumo mpya wa mambo duniani? Yaliyojadiliwa ni baadhi ya mapinduzi ya karne iliyopita, ikiishia katika kuinuka kwa USA, kuuawa kwa kennedy, na kuweka mfumo mpya duniani.

216SW - Uwingiliano na Uislamu
Added: 29th September 2014
Views: 3170
Comments: 0
Mada hii imekuwa fumbo kwa wachanganuzi wengi. Je uislamu inauingiliano upi na pambano hili la kimataifa. Je ni pambano la kisiasa, kidini ya mchanganyiko wa dini na siasa? Mwanzo wake ni upi na lengo lake nini? Je inaathiri vipi muungano wa makanisa na fundisho la wokovu katika kristo? Gundua hayo kutoka katika filamu hii. Mstari wazi huchorwa kihistoria, ukweli unashangaza kuliko dhana tuu.

217SW - Uhalifu Wa Vizazi Vyote
Added: 29th September 2014
Views: 2765
Comments: 0
Katika filamu hii kazi za kisiri ya mpinga kristo yanabainishwa- jinsi anvyojiketisha katika hekalu la Mungu akidai kwamba yeye ni Mungu na eti anazo nguvu kumzidi aliye juu, akidai kwamba anao uwezo wa kubadilisha amri ya Kristo. Maana ya mabadiliko ambapo dunia nzima inapotoshwa yamewekwa wazi. Mara nyingine tena, biblia na biblia pekee yake ndio yafaa kutumiwa kuziweka wazi kazi zake.

218SW - Wanyama Wawili Wamekuwa Marafiki
Added: 29th September 2014
Views: 3390
Comments: 0
Fundisho hili limetoka katika kitabu cha Ufunuo sura ya 13 linaeleza jinsi mnyama wa bahari na mnyama wa ardhi kuwa marafiki, kilele katika mfumo mpya wa ibada ambayo heshima mnyama wa kwanza. Kutoa ushahidi wazi juu ya utambulisho na malengo ya nguvu hizi kisiasa, mada hii ni pamoja na kuangalia United States katika unabii wa Biblia na umuhimu wa Kanisa na hali kujitenga.

219SW - Mvinyo Wa Babiloni
Added: 29th September 2014
Views: 2853
Comments: 0
Bibilia inazungumzia babiloni ya siku za mwisho itakayoipotosha dunia. Mafundisho ya mamlaka haya ya siku za mwisho yanapatikana katika babiloni ya zamani. Katika filamu hii, dini ya zamani ya babiloni na mwanzo wake yanafuatiliwa kupitia nyakati za historia hadi kwa wakati wetu huu. Inabainishwa wazi jinsi ambavyo dini ya kale ipo hai katika mifumo za kidini za wakati wetu, ikijivika mavazi yanaifanya kufijificha kutokana na watazamaji wa kawaida.

220SW - Mwanamke Aliyemkalia Mnyama
Added: 29th September 2014
Views: 2955
Comments: 0
Filamu hii ni uchambuzi wa ufunuo 17 inayoeleza mwanamke anayedhibiti muungano wa nguvu. Mwanamke anazosifa za dini ya siri ya babiloni, nayo inawashawishi dunia kufuata amri yake. Uchambuzi wa kina inawakilishwa ikilinganisha mtazamo wa jumla kuhusu sura hii na ukweli wa siku za leo. Sura hii inatayarisha kwa matukio ya mwisho katika pambano kati ya wema na uovu.

-